Umejifunza Nini Kuhusu Hili la Ronald na Lionel Messi....Mfano wa Ali Kiba na Diamond

Cristiano Ronaldo anasema licha ya kuwa na upinzani mkubwa na Lionel Messi katika mpira wa miguu mahusiano yao yapo sawa yani hawana tatizo.

Ameongeza kuwa sio kitu rahisi kwa watu wawili wanaoshindana kusimama kwenye jukwaa moja katika kipindi kisichopungua miaka 15 huku kila mmoja wao akimpa hamasa mwenzake kushindana.

Ronaldo pia amegusia jinsi ambavyo anamis kucheza Laliga ambapo wamekuwa na ushindani mkubwa na Messi amekiri pia licha ya ukaribu wao na kuwa na mahusiano mazuri hawakuwahi kujumuika pamoja kwenye chakula cha usiku akitaraji kufanya hivyo kwenye siku za usoni pengine.

Umejifunza nini...? Hapa Kwetu tuna Diamond na Ali Kiba ila hawawezi kula chungu kimoja kila mmoja anavimba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad