Umeme Wamponza Kiongozi Ashushwa Cheo na Waziri wa Nishati


Kufuatia hitilafu ya kukatika kwa umeme kulikotokea asubuhi ya Agosti 1 katika maeneo mbalimbali ya nchi, msimamizi wa nguzo kubwa za umeme ameshushwa cheo kwa kile kilichoelezwa kwamba Serikali haiwezi kufanyakazi na watendaji wazembe.


Agizo hilo la kushushwa cheo limetolewa na Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani baada ya kuonyesha kutoridhishwa na taarifa ya hitilafu hiyo, iliyosababisha taharuki kwa wananchi.

Waziri Kalemani akizungumza mara baada ya kutembelea nguzo hizo zilizo mbali kidogo na mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi, amesema Serikali haiko tayari kufanyakazi na watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

Akielezea tatizo liliotokea, Mhandisi Msimamizi aliyoteuliwa na Dkt. Kalemani kushika nafasi hiyo, Mhandisi Samson Ngunga ameahidi kutafuta ufumbuzi wa hitilafu hiyo ya umeme haraka iwezekanavyo.



Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yes...!!! Kalemanni uko sahihi kabisa
    Non Performa ingekuwa Wizarani kwangu niNje tuuuu. Muda wa kubembeleza umesha pitwa naa wakati Mtanzania kwa sasa anachotaka ni kuona sisi tunajituma vipi kumtatulia Adha za maisha yake ya kila siku.
    Na Ajira tunao vijana wengi wabunifu
    who can Perform even better they need our trust .

    Huyo ana bahati kushushwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad