Unaambiwa MALAYA Morogoro Wamwaga Radhi KITUO Kikuu Cha Polisi


WANAWAKE wapata 36 wakazi wa maeneo mbali mbali Mkoa hapa,wamezua balaa la aina yake ‘Kuchomoa betri’ kwenye kituo Kikuu cha Polisi Morogoro, baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya biashara haramu ya kuuza miili yao.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo katika nyakati tofauti Polisi waliwadaka dada poa hao maeneo ya Kahumba katikatika ya Mji wa Morogoro na ltigi iliyopo maeneo ya Msamvu wakiwa mawindoni nyakati za usiku jambo ambalo mara kwa mara lilikuwa likipigiwa kelele na nyombo vya dola.

Hivyo ili kuwadhibiti dada poa hao wiki end iliyopita ljumaa na jumamosi jeshi la Polisi lilifanya msako mkali kwenye kumbi hiyo na kufanikiwa kuwadaka wanawake hao na kuwasweka mahabusu ambapo jumatatu walipelekwa mahakamani.

Wakiwa kituo cha polisi wanawake hao wakihojiwa na Mwandishi wa Mtandao huu walidai kwamba wamelazimika kufanya biashara hiyo haramu baada ya mabwana zao kuungua na Moto katika ajali ya Lori la mafuta iliyotokea Agost 10 Msamvu jirani na eneo la ltigi.

Akizungumza na Mtandao huu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroldi Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa dada poa hao 36.

Katika hatua nyingine Machangu hao walipotoka mahabu na kupanda difenda tayari kuelekea mahakama walipomuona Mwandishi wa Mtandao huu anawapiga Picha waliweka mapozi kama wanashiriki shindano la Umisi.

”Mwandishi shida yako si picha haya tunaweka pozi tupige picha ukauze kwenye magazeti yako sisi hatujaua tunauza miili yetu wenyewe ili tupate pesa za matumizi”walisema dada poa hao amabo wengi wao ni watoto wa mjini wanamfahamu vyema Mwandishi wa habari hizi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad