Upinzani Wang’aka, ‘Hatususii Uchaguzi’

Upinzani wang’aka, ‘Hatususii uchaguzi’
Vyama vya Upinzani nchini vimesema kuwa haviwezi kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kutokana na figisu wanazofanyiwa.

Akizungumzia hali hiyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Alliency For Democratic Party (ADC), Doyo Hassan Doyo amesema kuwa kususia suala la uchaguzi sio sahihi.

Amesema kuwa ni lazima mapambano yaendelee kwani upinzani ungekata tamaa katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015 basi kusingekuwepo na wabunge wa upinzani kwasasa.

Aidha, amesema kuwa ni lazima wao kama wanasiasa kuendeleza mapambano hata kama wasipofaidika lakini historia itaendelea kuwakumbuka kwaajili ya vizazi vijavyo.

”Ni kupambana tu kufa na kupona uchaguzi unaokuja unaweza kuwa mgumu kuliko chaguzi zote kwani CCM imejipanga kuweka mapingamizi  kwa wagombea, ambapo mtendaji kata au mkurugenzi akikubali matokeo ndio basi tena,”amesema Doyo

Kwa upnde wake, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha ACT- Wazalendo, Msafiri Mtemelwa amesema kuwa kwa mazingira yaliyopo ni kama hakuna uchaguzi ila zinafanyika ili kuwaonyesha wafadhili kuwa kuna uchaguzi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Eugen Kabendera amesema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu ni lazima upinzani ushiriki licha ya figisu zilizopo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad