Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema kuwa umetuma maombi Caf ili kuweza kupata leseni za wachezaji wao wa kimataifa, Farouk Shikalo, Maybin Kalengo na David Molinga ‘Falcao’ ili waweze kucheza mchezo wa marudiano.
Wachezaji hao watatu wa Yanga wa kimataifa walikosa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers kutokana na kukosa leseni.
Fredrick Mwakalebela ambaye ni Makamu Yanga yapeleka barua Caf Khadija Mngwai na Marco Mzumbe Mwenyekiti wa Yanga, amesema: “ Tumefanya mazungumzo na Caf kwa njia ya email ili watupatie leseni za wachezaji wetu watatu ili tuwatumie kwenye mchezo wa marudiano na Township.
“ ITC za wachezaji wetu wote tumeshazipata kutoka katika klabu ambazo wachezaji walikuwa wakichezea ila tatizo ni leseni ambazo tulizikosa kutokana na wachezaji kusajiliwa katika dakika za mwisho.
Sio kwetu peke yake kutokea jambo hili, bali ni kwa timu zote zilizochelewa kufanya usajili kutokana na kuwahi kuanza kwa mashindano haya.”