Uwanja wa Ndege JNIA Watusua, Waingia ‘top 10’ Afrika



Zaidi ya abiria milioni nane watahudumiwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kukamilika kwa jengo la tatu la abiria (Terminal III), huku jengo hilo jipya likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Uwezo wa kuhudumia abiria hao kwa mwaka unaufanya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuingia katika viwanja kumi Afrika vyenye uwezo wa kuchukua abiria wengi.

Sehemu ya huduma mbalimbali kwa Wasafiri iliyopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataiafa Julius Nyerere Terminal 3, Jijini Dar es Salaam ambao ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.

Jengo la kwanza la abiria (Terminal 1) lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka wakati jengo la pili (Terminal 2) likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

Hata hivyo, jengo la Terminal 2 ambalo ndilo linatumika kwa sasa limekuwa likilemewa na wingi wa abiria mpaka kufikia milioni 2.6 kwa mwaka.


Sehemu ya Ukaguzi mizigo kwa abiria yenye miundombinu ya kisasa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataiafa Julius Nyerere Terminal 3, Jijini Dar es Salaam.
Kukamilika kwa jengo la tatu la abiria kutapunguza msongamano wa abiria kwenye jengo la pili na kurahisisha shughuli za usafiri wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia mradi huo jana Alhamisi Agosti Mosi, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanywa na Rais John Magufuli, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale alisema wazo la kujenga uwanja huo lilikuja baada ya jengo la pili kuelemewa na wingi wa abiria.

Sehemu inayotumika kwa abiria kuingia na kutoka kwenye ndege yenye miundombinu ya kisasa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kama inavyoonekana kwenye picha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad