Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, Unafurahije Wakati nchi yako imepata Majanga. Hawa ni ma Munda, ma Sadist or What?



Jumatatu ya leo, nimeipata tena fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa. Leo nazungumzia Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, nchi yako inapatwa na majanga, halafu wewe unafurahi, huu ni Uzalendo wa aina gani?. Kiukweli huu ni Uzalendo wa Ajabu Kabisa kuwahi kutokea.


Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, Nchi Yako Inatukanwa!, Rais Wako Anatukanwa!, Tumenyamaza!. Huu Ni Uzalendo Gani?

Wanabodi, Makala za Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla. Naendelea na Makala zangu ziitwazo Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la kila siku za Jumatatu. Hizi Makala zitafuatiwa na Kipindi cha TV chenye jina hilo hilo ambacho kitaanza kutoka kwenye...


Baada ya kupatikana taarifa ya kakamatwa kwa ndege yetu na kuzuiliwa nchini Africa Kusini, kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wanafurahia kakamatwa kwa ndege hii, hawa ni watu wa ajabu sana.

Mtoto ukiwa unamchapa sana, anakuwa sugu, anakuwa nunda, anakuwa yuko tayari kufanya lolote bila kujali atachapwa au laa. Hivyo inawezekana huku kubana kwa vyuma kumewafanya baadhi ya Watanzania wenzetu kuwa manunda wanafurahia majanga kwa taifa lao?.

Mtu yoyote anayefurahia majanga ya mwingine, huyu ni sadist, anapata gratification kwa mateso ya wengine, inawezekana baadhi ya Watanzania wenzetu wamekuwa ma sadist kiasi cha kufurahia majanga kwa taifa lao?




Kufuatia hali hii, sisi Tanzania kama taifa tuna haja ya ku redefine, Uzalendo wetu kwa taifa letu kwa kufanya kampeni ya uhamasishaji Uzalendo, kupitia vipindi vya uhamasishaji Uzalendo kwa civic education ya kutenganisha matukio ya kitaifa na matukio ya kisiasa.

Japo rais Magufuli ni mwana CCM na aligombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, na baada ya kushinda ni CCM ndio imeshinda na kuunda serikali, hivyo ni serikali ya CCM, hivyo kuna watu wakiwemo wapinzani wanamuona rais Magufuli kama ni rais wa CCM na kuihesabu serikali ya Tanzania kama ni serikali ya CCM, hivyo kwao kila kitu kinachofanywa na serikali, kwa ni kwa ajili ya CCM, hivyo mafanikio yoyote ya rais Magufuli na serikali yake, wanayahesabu ni mafanikio ya CCM, hivyo nchi ikikutwa na majanga yoyote, wao wanashangilia wakihesabu ni majanga kwa CCM.

Ukweli ni kuwa, japo mgombea anadhaminiwa na chama cha siasa, na kupendekezwa na chama cha siasa, baada ya kupitishwa na NEC kuwa mgombea, huyu sasa anakuwa ni mgombea wa taifa na anachaguliwa na Watanzania wote na sio watu wa chama chake.

Akiisha chaguliwa, anakuwa ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa wote na sio kiongozi wa chama chake.

Hivyo rais Magufuli japo ni mwana CCM, sio rais wa CCM, ni rais wa Watanzania wote wakiwemo hao wapinzani, hivyo majanga yoyote yatakayoikumba nchi sio majanga kwa rais Magufuli, na serikali yake, sio majanga kwa serikali ya CCM, ni majanga kwa Tanzania nzima kama nchi na watakao athirika na majanga haya sio rais Magufuli na serikali ya CCM, bali ni rais Magufuli na serikali ya Tanzania na nchi nzima ya Tanzania kama taifa tukiwemo sisi Watanzania wote individual, uwe ni CCM, upinzani, huna chama, ni mkulima, hupandagi ndege, nchi ikikumbwa na majanga kama hili la kukamatwa na kushikiliwa kwa ndege yetu, ni janga la kitaifa, sote tutaathirika.

Uzalendo wa kweli kwa nchi yako ni pamoja na kuitakia mema na mafanikio regardless ni chama gani kiko madarakani, maendeleo hayana vyama, na Uzalendo wa kweli wa taifa lako pia hauna vyama, janga lolote la taifa ni janga la wote, mzalendo wa kweli wa taifa lake hawezi kufurahia majanga yoyote kwa taifa lake regardless ni chama gani kiko madarakani.

Jumatatu Njema
Paskali
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad