Venezuela yalaani vikwazo vipya vya Marekani


Venezuela imekosoa vikali vikwazo vipya vya Marekani dhidi yake, ikivitaja vikwazo hivyo kuwa ''ugaidi wa kiuchumi''.

Wizara ya mambo ya nje mjini Caracas imesema tayari vikwazo vya awali vya Marekani vimesababisha madhara makubwa kwa jamii ya Wavenezuela.

Jumatatu wiki hii, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza vikwazo vipya dhidi ya Venezuela, ambavyo vinashikilia mali zote za serikali inayoongozwa na Rais Nicolas Maduro zilizoko nchini Marekani.

Kwa miezi kadhaa sasa, kumekuwepo uwaniaji wa madaraka baina ya Rais Maduro na kiongozi wa bunge la Venezuela Juan Guaido ambaye alijitangaza rais wa mpito.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad