VIDEO: Alichokisema aliyenusurika katika ajali ya ndege


Dar es Salaam. Mmoja wa abiria wanane walionusurika katika ajali iliyotokea juzi Mafia, amesema ndege hiyo iliacha njia na kugonga ukuta wakati ikiwa katika njia ya mwendo wa kasi kuelekea kupaa.

Ndege hiyo ya kampuni ya Tropical ilipata ajali wakati ikiondoka Uwanja wa Ndege wa Mafia mkoani Pwani kuelekea jijini Dar es Salaam.

Hadi jana jioni Jumatano Agosti 7, 2019 abiria huyo, Hassan Bakari na wenzake watatu walikuwa wamelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa (Moi) baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mafia juzi kutokana na kupata majeraha makubwa.

Watu sita kati ya tisa waliokuwa kwenye ndege hiyo walijeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha, kwa mujibu wa kamanda wa polisi Rufiji, Onesmo Lyanga.


Bakari, ambaye amepata majeraha ya moto usoni, mikononi, shingoni na kifuani, aliiambia Mwananchi jana kuwa wakati ndege hiyo ikishika kasi kwa ajili ya kuruka, ilihama njia na kugonga uzio.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad