Viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan kuapishwa leo


Viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan wanatarajiwa kuapishwa hii leo, ambapo baraza huru litaongozwa na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ambaye ni mkuu wa baraza la jeshi la mpito ambalo limeongoza Sudan tangu April mwaka huu wakati jeshi lilipomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu nchini humo, Omar al-Bashir.

Msemaji wa baraza la jeshi linalotawala nchini Sudan amewaambia waandishi wa habari kwamba nchi hiyo ilikamilisha mfumo wa baraza huru lenye wanachama 11 ambao wataongoza serikali ya mpito nchini humo kwa kipindi cha miaka mitatu hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.

Wiki iliyopita ushirika unaoongoza upinzani ulimteuwa mchumi, Abdalla Hamdok kuhudumu kama Waziri Mkuu katika serikali ya mpito nchini humo.

Aidha, mkataba wa kushirikiana madaraka pia unakubali wabunge 300 wa baraza la wawakilishi kuhudumu wakati wa kipindi cha mseto na baraza la mawaziri lenye wasomi.

Hata hivyo, Changamoto kubwa kwa serikali mpya itakuwa matatizo ya kiuchumi kutokana na kushuka kwa thamani kwa sarafu ya kigeni na kusababisha maisha kuwa magumu kwa wakazi wa nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad