Waajiri Wanaonyima Likizo za Uzazi Kuchukuliwa Hatua
0
August 02, 2019
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetangaza kuwachukulia hatua Waajiri wote wanaovunja Sheria kwa kugandamiza haki ya kupata likizo ya uzazi kwa wanawake pindi anapojifungua
-
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma
-
Waziri Ummy amesema “Haki ya Mwanamke Kuzaa na kupata likizo ya uzazi ni haki yake ya asili, haitakiwi kuwekewa vikwazo, kwahiyo nitoe wito kwa Wanawake wanaofanya kazi, ni haki yako kupata likizo.”
-
Ameongeza kuwa “Mwanamke Asije mtu akakwambia anaijaza kazi yako kwakuwa umetoka likizo ya kujifungua. Tuambie sisi, tutachukua hatua, na huyo Mwajiri tutamtangaza kuwa ni adui wa Wanawake na Watoto wa Tanzania.”
-
Aidha, Waziri Ummy amebainisha kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuanzisha dawati la kutoa malalamiko litaloshughulikia kupigania na kutetea haki za wanawake kupata likizo ya uzazi