Wafanyakazi wa UN Wachunguzwa kwa Ubadhirifu

Wafanyakazi wa UN Wachunguzwa kwa Ubadhirifu
Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Associated Press umegundua kwamba baadhi ya wafanyakazi wa misaada waliopelekwa Yemen taifa linalokabiliwa na mzozo wa kibinaadamu kufuatia vita vya miaka mitano wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa misaada ya chakula, dawa na fedha.

Nyaraka kutoka uchunguzi wa ndani wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO, zimefichua madai ya mamilioni ya dola yaliyoingizwa kwenye akaunti binafsi za wafanyakazi hao, mikataba inayotiliwa shaka na tani za madawa ya misaada yaliyotumika kinyume na malengo ama kutojulikana zilipo.

Shirika hilo la habari la AP liliwahoji watumishi wanane na maafisa wa zamani wa serikali na wakaguzi wa ndani wanaochunguza madai hayo pamoja na watumishi wasio na sifa kuajiriwa katika nafasi za juu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad