Wafanyakazi watatu wa kampuni ya tigo mbaroni kwa utakatishaji fedha
0
August 02, 2019
Wafanyakazi watatu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na wafanyabiashara wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita likiwemo la kutakatisha fedha sh. Milioni 20.3.
Mashtaka mengine ni, kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,kuingilia mifumo ya kifedha ya Tigo pesa bila kibali, kupatikana na mavazi ya JWTZ.
Wafanyakazi wa Tigo ambao wanashtakiwa katika kesi hiyo ni, Kokubelwa Karashani, mtoa hudumu kwa wateja, Godfrey Magoye, wakala na Khalfan Milao mtoa huduma kwa wateja. Wengine ni Mohamed Abdallah mfanyabiashara na Moses Kilosa.
Akisoma hati ya mashtaka wakili Wa serikali Mwandamizi Simon Wankyo ambele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine RwiIzile amedai kuwa, Siku na mahali pasipojulikana washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Katika shtaka la pili imedaiwa, Kati ya Januari Mosi 2018 na Juni 20,2019 katika maeneo tofauti Kati ya Dar es Salaam na Arusha washtakiwa hao walijipatia sh. 20,378,627 mali ya wateja wa kampuni ya Tigo ambazo walizitoa kutoka Tigo Pesa bia kuwa na kibali Chao.
Mshtakiwa Abdallah peke yake anadaiwa, Juni 10,2019 huko Kinyerezi mtaa wa Kibaga wilaya ya Ilala, alipatikana na mavazi ya serikali ambayo ni Koti moja, suruali moja, pingu na kofia moja Mali ya jeshi la wananchi JWTZ.
Pia imedaiwa kati ya Januari Mosi 2018 na Juni 20, 2019 huko katika ofisi za Tigo Shop zilizopo Mlimani City mshtakiwa Kokubelwa akiwa kama mtoa huduma wa idara ya huduma kwa wateja aliingilia mfumo wa kifedha wa wateja wa Tigo na kutoa taarifa kwa Mohamed kwa lengo la kujipatia fedha kwa wateja wa Tigo.
Mshtakiwa Godfrey anadaiwa akiwa wakala wa Tigo pesa huko Kariakoo Tigo shop, kwa udanganyifu aliingilia mifumo ya kifedha ya wateja wao bila taarifa na kutoa taarifa za wateja kwa Mohamed Abdallah.
Katika shtaka la utakatishaji imedaiwa washtakiwa walitakatisha fedha hizo, sh. Milioni 20.3 huku wakijua kuwa fedha hizo ni mazalia ya pesa tangulizi ya kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka yao hawakutakiwa kujibu Hata hivyo wakili Wakili wa Wankyo amesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. kwa kuwa makosa hayo ni ya uhujumu Uchumi na mahakama hiyo haina na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakalimia.
Aidha, wakili Wakili Wankyo amedai, wako katika hatua ya kuwasilisha maombi mahakamani hapo kuomba kampuni ya Tigo itoe taarifa zote ili kusaidia upelelezi kukamilika haraka kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa na tabia ya kusua sua kutoa taarifa zinazoweza kusaidia kwenye upelelezi. Kai hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13, mwaka huu.
Tags