Wakamatwa na Polisi kwa kuiba mafuta baada ya lori kuanguka

Watu wanane wilayani Ngara mkoani Kagera wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi wa mafuta katika gari lililopata ajali Kijiji cha mshikamano maarufu kama machinjioni ajali ambayo ilisababisha kifo cha dereva wa gari hilo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema licha ya kukamatwa watu hao pia wamefanikiwa kukamata lita 300 za mafuta zilizokuwa zimeibiwa katika tukio hilo.

Shughuli za ufaulishaji mafuta zikiendelea chini ya ulinzi mkali wa jeshi la police katika eneo la ajali iliyotokea Jana katika eneo la machinjioni kabla ya kufika mpaka wa Rusumo wilayani Ngara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad