Wakazi aeleza tatizo la wana HipHop kutojua kuvaa

 
Mwana HipHop Wakazi, ameeleza sababu za wasanii wa muziki huo kutozingatia mavazi ili kupata pesa na suala la kuingia kwenye siasa na uongozi.


Wakazi amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuhusu wasanii wa HipHop kutotumia mionekano yao kutengeneza pesa.

"Mionekano ipo ya aina mbalimbali, kumbuka hata Mrisho Mpoto kuwa pekupeku ndiyo kuna muingizia pesa, kuna muda tusilazimishe kwamba muonekano ndiyo unakuingizia pesa kwa sababu kama Mwana HipHop unaweza kijitengenezea njia zako zingine na bado ukapata pesa", amesema.

Aidha Wakazi ameendelea kusema kujiweka kibiashara ni muhimu hata kama unavaa vibaya, lakini zaidi ya muonekano unaweza kupata pesa kutokana na unavyojiwakilisha, unachozungumzia kwenye muziki, maisha yako na mitandao ya kijamii.

Pia Wakazi amesema hajawahi kuongea na Mwana Fa na Nikki Wa Pili kuhusu kuingia kwenye siasa licha ya majina yao kutajwa sana kuingia kwenye siasa.

Hata hivyo amesema anapenda na yupo tayari kuwa kiongozi kwa sababu anatoa akili za maisha kwa vijana, anatoa njia za ufanyaji kazi na kusisitiza watu kuhusu maadili.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad