Wakimbizi 2,000 nchini Tanzania kurudishwa Burundi kila wiki


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Burundi, Pascal Barandagiye, wamesaini makubaliano ambayo watahakikisha wakimbizi wote waliopo katika kambi hizo wanarejeshwa nchini kwao huku akiwaonya watu au mashirika yatakayokwamisha juhudi hizo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi, Pascal Barandagiye, wakisaini maazimio ya makubaliano ya kuwarejesha wakimbizi 2,000 kila wiki nchini kwao.


Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Kigoma, Waziri Lugola amesema makubaliano hayo yataanza rasmi Oktoba Mosi na wakimbizi hao watakuwa wanarejeshwa nchini mwao na kupata mapokezi makubwa na serikali ya Burundi.

“Tuna taarifa wapo baadhi ya watu, mashirika ya kimataifa wanawarubuni wakimbizi wakiwatangazia kuwa Burundi haina amani, jambo ambalo si la kweli, nchi hiyo ina amani na wakimbizi wanapaswa kurejea nchini mwao,” amesema Kangi Lugola na kutoa onyo kwa watakaokwamisha zoezi hilo.

“Natoa kauli hii sio kuwatisha au kutishia nyau, bali nasema, serikali ya Magufuli haiwezi kuchezewa na mtu yeyote, hivyo tutawakamata wanaowarubuni, wanaowashawishi wakimbizi wasiende nchini mwao,“.

Waziri Lugola katika hilo, Amesema watatekeleza makubaliano ya  pande hizo tatu ambazo ni Serikali ya Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)  kurudisha wakimbizi 2,000 kila wiki kwenda Burundi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad