Wanafunzi vyuo vikuu hawajui kuoga- Dkt Shule


Mhadhiri wa Kitivo cha Sanaa ya Ubunifu, Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Vicensia Shule, amewaomba wazazi kuwajengea watoto wao ujuzi wa masuala ya usafi na kujitegemea kuanzia ngazi ya chini ili kuwaepusha kuwa mizigo isiyobebeka.


Dkt Shule ameyabainisha hayo leo Agosti 16, katika kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, ambapo amesema vijana wengi wanaotoka katika familia ambazo hazina mfumo mzuri wa malezi kwa watoto ndiyo wanaoongoza kwa uchafu na uharibifu wa mali maofisini.

"Utakuta mtoto ana kisigino cheusi, kesho ukimpa gari la Ukurugenzi huyu si atalipandisha mkaa, kwa sababu hajatokea katika familia aliyofunzwa kujitegemea na kujua uchungu wa vitu, kwa sababu mambo mengi wanafanyiwa", amesema Dkt Shule.

Aidha Dkt Shule ameeleza athari ya malezi mabovu kwa mtoto, ambayo inapelekea watoto kubweteka hata wanapofika ngazi za vyuo kwa kuamini kuwa kila kitu wanaweza kufanyiwa na wazazi wao.

"Mimi nafundisha pale chuoni asilimia kubwa ya wanafunzi hawajui kuoga, nafundisha masomo ya kuigiza pale mwanafunzi utakuta ananuka mpaka aibu'' amesema Dkt Shule.

Ikumbukwe kuwa Dkt Shule ndiye Mhadhiri aliyezua gumzo na mjadala mitandaoni juu ya kukithiri kwa  uwepo wa rushwa ya ngono katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka uliopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad