Moja kati ya vitu ambavyo mashabiki tulivipokea kwa furaha sana ni hatua ambayo @diamondplatnumz
alipoamua kuanzisha lebo ya #WCB lengo kubwa lilikuwa ni kuinua sanaa ya Tanzania na kuwapa nafasi
vijana wenzake waliopo mtaani. Watanzania tulilipokea kwa mikono miwili na mpaka sasa Wasafi ndiyo
lebo kubwa ya muziki Afrika Mashariki na kati hili halina ubishi
.
.
Lakini ndani ya miezi miwili mitatu hii kumekuwa na sintofahamu juu ya kinachoendelea kati ya uongozi
wa WCB na mtoto wenu wakwanza kimuziki @harmonize_tz Uvumi ni kuwa uongozi na msanii wao hawapo sawa japo kila mtu anajaribu kukwepa kuanika ukweli. Tetesi zaidi zilianza kuvuma baada ya kumkosa @harmonize kwenye
baadhi ya mikoa inapofanyika tamasha la Wasafi Festival. Inawezekanaje msanii aliyeko chini ya lebo kama Harmonize afanye show moja tu ya Wasafi Fesival?, inamaana uongozi haukuwa na ratiba ya
msanii mpaka apate mkoa mmoja tu na iko wazi kuwa Harmonize ni miongoni mwa wasanii pendwa
zaidi kwenye lebo ya WCB?. Mashabiki tunaumia juu ya hili tupo njiapanda
.
.
Mzazi akikosea hasemwi kwa hali ilivyo sasa mashabiki tunamnyooshea kidole @harmonize_tz kila kukicha. Kinachofuata ni matusi kwenye ukurasa wa Harmonize je kama uongozi mmelitafakari hili?. Msanii anayaoga matusi kila kukicha hamuoni kama mnavunja kitu mlichokijenga
kwa miaka mingi?, @babutale @sallam_sk @diamondplatnumz mko wapi kutoa maelezo ya kina kwa
mashabiki?.
.
.
Pia inasemekana kuwa (Taarifa zisizo rasmi) meneja wa Country Boy @petimanwakuache alikutana na maneno makali baada ya kushutumiwa kwamba alitaka kumpandisha Harmonize kama Surprise kwenye tamasha la Wasafi Festival Dodoma. Sasa kwa hali hii tutafika?, WCB mnanguvu kubwa kwenye muziki wa Tanzania na tunawategemea sana sasa kama mnaanza kuvuruga mashabiki wapi tutaelekea?, jitafarini juu ya hili kama ni kiki mnaitengeneza basi jueni hasara zake ni kubwa kuliko faida
.