Washika vibendera katika soka nafasi zao kuchukuliwa na maroboti

 


Shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu duniani (FIFA) limeripotiwa kuwa kwa sasa linafikiria uwezekano wa kuwaondoa washika vibendera katika mechi (linesmen) na nafasi zao kuchukuliwa na maroboti. 


Mtandao wa Mirror wa nchini England unaeleza kuwa hadi sasa FIFA wana kitengo maalum kinachofanya uchunguzi na kushughulikia kwa undani zaidi kama wanaweza kuwaondoa washika vibendera na wakaanza kutumia teknolojia kuamua mpira wa kuotea (offside) na mipira ya kurusha. 


"FIFA tayari imeshakuwa na hiki kitengo cha uchunguzi kuhusiana na hili suala, waamuzi wasaidizi majukumu yao yatekelezwe na Camera na computer kuongoza offsides na mipira ya kurusha" kilisema chanzo ambacho jina lake limehifadhiwa. 


Kama teknolojia hiyo itakubalika na kuwa kweli basi watu wa familia ya soka ambao wamekuwa wakiipinga VAR hawatafurahishwa nayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad