Watu 45 wakamatwa kwa tuhuma za kushambulia kwa mawe msafara wa DC Kyela, Yadaiwa walitaka mama amfufue mwanae aliyefariki

Watu 45 wamekamatwa na jeshi la polisi Wilayani Kyela, Kwa tuhuma za kushambulia kwa amwe msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya uliokuwa unaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya, katika kijiji cha Mpunguti, Kata ya Makwale.


Chanzo cha vurugu hizo, Imeeleza kuwa kulikuwa na mtu alifariki kwenye uwanja wa mpira, Na wananchi wakawa wanahisi Mama yake mzazi ndiye aliyemuua kwa imani za kishirikina hivyo maiti ilipotaka kuzikwa wakakataa wakimtaka Mama yake amfufue.

Wakati vurugu hizo zikiendelea, Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na DC walikuwa maeneo hayo katika ukaguzi wa masuala ya Mwenge na mitihani, Hivyo waliposikia taarifa za mama  huyo wakapita kusuruhisha ndipo wananchi wakafunga njia na kuanza kuupopolea mawe msafara wa Mkuu huyo wa Wilaya.

“Mpaka sasa DC na wenzake wako salama hali ya amani na utulivu imerejea mimi nipo eneo la tukio, kuna bwana amefariki kwenye uwanja wa mpira wananchi wakawa wanahisi mama yake mzazi amemuua kwa imani za kishirikina, maiti ilipotaka kuzikwa wakakataa wakamtaka mama yake amfufue,” amesema Kamanda Ngowi .

Kamanda Ngowi,  amesema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wale wote  waliohusika kwenye tukio hilo na hakuna hata mtu aliyeumizwa licha ya kuwa kulikuwa na vurungu nzito.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad