Katika mahusiano ya mapenzi pamoja na kuwapo kwa sababu mbalimbali zinazochangia mpenzi mengi kufa lakini zipo sababu nyingine ikiwemo watu wanakuzungukua huwa ni chanzo cha kufa kwa mahusiano ya kimapenzi kufa.
Wafutao ndiyo watu wanachangia kufa kwa mahusiano;
Wapenzi wa zamani.Hili ni grupu la kwanza la watu wanaovunja mahusiano ya watu wengi na kama sio kuvunja basi kupelekea ugomvi,,usipende kuwa na mawasiliano na ma ex wako hata kama mliachana pasipo na ubaya wowote maana mpenzi wako anapogundua kuwa unawasiliana nae hii inajenga wasiwasi ndani ya moyo wake na wengi hawapendi.
Wafanyakazi wenzako.Hawa nao ni watu unaoweza kuwachukulia kawaida kwasababu tu unafanya nao kazi lakini hawa pia wanachangia,,,utasikia fulani twende lunch,,siku ya kwanza,ya pili,ya tatu mwisho wa siku mnapanga kutoka dinner na mwisho wa siku unamcheat mpenzi wako bila kutegemea.
Majirani.Hawa nao ni watu ambao sio wazuri kwasababu ya maneno,,huyu leo atazusha hili kesho lile,,na kwa upande mwingine hasa hasa wanawake akimpenda mume wa mtu ataanza kumuwekea mitego ili amnase,,wanaume kuweni nao makini hawa watu na usijenge mazoea nao yakupitiliza.
Wafanyakazi wa ndani.Hawa ni kitu cha kawaida sana kuharibu ndoa za watu na wengine kufikia mpaka kubeba mimba ya baba mwenye nyumba,,mwanamke hakikisha housegirl hamfulii mumeo wala kumpikia maana wengine ndo wataweka na limbwata ili wakupindue lakini muda mwingine inakuwa ni tamaa tu za wanaume.
Marafiki.Marafiki ni watu ambao wanaweza kukushape vizuri au vibaya,,hivyo kuwa makini na ushauri au mawazo ya marafiki,,si kila kitu unacopy au unafata toka kwa marafiki
Ndugu.Jamaa na ndugu ni wabaya sana usipokubalika,,wasipokupenda basi watakufanyia kila aina ya vituko ili tu uachane na ndugu yao.
N.b;kuwa makini na watu huwa.