Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa jeshi la polisi linawashikilia watu 3 kwasababu ya maandamano yasiyo na kibali wakishinikiza kurejeshwa kwa ndege ya Tanzania inayoshikiliwa Afrika Kusini.
Mambosasa ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wananchi hao walikuwa wakielekea Ubalozi wa Afrika Kusini, kwa ajili ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ambayo inashikiliwa na Serikali ya Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama.
“Kwanza sisi Jeshi la Polisi haturuhusu maandamano, na pia haturuhusu mtu kufanya anavyojisikia yeye, baada ya kupata taarifa nilimwagiza RPC ilala ili kuchukua hatua za kuzuia maandamano pili kuwakamata waratibu wa maandamano hayo.”amesema Kamanda Mambosasa
Kwa sasa nchini Afrika Kusini kuna ndege ambayo ni mali ya Tanzania inashikiliwa kutokana na kuwepo kwa kesi ya muda mrefu inayomhusisha mkulima mmoja ambaye alikuwa akiishi Tanzania kufuatia kutaifishwa kwa mali zake alipokuwa akiishi Tanzania.
Watu watatu wakamatwa kwa kushinikiza ndege ya Tanzania iachiwe
0
August 28, 2019
Tags