Mtoto mmoja nchini Indonesia amepewa jina la Google na wazazi wake kwa ajili ya kupata umaarufu na bahati kama ilivyo kwa mtandao wenyewe wa Google.
Jina hilo amepewa na Baba na Mama yake mzazi na wala hatotumia majina matatu kama ilivyo kwa biandamu wengine ambavyo wanatumia.
Baba wa mtoto huyo ambaye ana miezi minane kwa sasa, aitwaye Andi Cahya Saputra(31), amesema kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo kuwa, “wazo la kumpa mwanaye jina hilo lilikuwa tangu mke wake alipokuwa na ujauzito wa miezi saba kwa mtoto huyo”.
Pia amesema ilikuwa ni changamoto kumpa jina hilo kwa sababu walipanga kumuita majina mengi yanayohusu makampuni ya vitu vya teknolojia kama vifaa vya simu, kompyuta, Windows, iPhone, Microsoft na Ios.
Aidha mama wa mtoto huyo aitwaye Ella Karin (27) amesema mwanzo hakulipenda jina hilo ila hatimaye alikubali kwa sababu linamaanisha ni moja kati ya mtandao unaongoza kwa umaarufu na kutembelewa na watu wengi zaidi duniani.
Mama wa mtoto huyo ameendelea kusema anamatumaini mwanaye huyo atakuwa kiongozi wa watu wengi kama ilivyo kwa mtandao wa Google wenyewe.