Waziri Jafo Atoa Maagizo Kwa Wakuu Wa Mikoa Na Makatibu Tawala Mikoa Kote


Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa,na Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kuhakikisha wanasimamia vyema mpango kazi wa Taifa wa uendelezaji wa Miji ili kuepuka ukuaji wa Makazi Holela.

Waziri Jafo ametoa Maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Mpango kazi wa wa Taifa wa  Maendeleo ya Miji Tanzania .

Waziri Jafo amesema suala la mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania itakuwa ajenda ya Kitalii na itakuwa na faida kubwa ikiwa ni pamoja na urahisi wa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kupitikika kwa maeneo kwani amesema kuna baadhi ya Mitaa haipitikiki kutokana na Makazi holela  hali ambayo husababisha hata magari ya zimamoto kushindwa kutoa huduma vizuri.

“Unakuta nyumba zimekaa kiholela hata gari la zimamoto linashindwa kutoa huduma vizuri na hali ambayo inasababisha kuteketea kwa watu pamoja na mali,maeneo mengine ni ya kusikitisha sana hata kupitisha jeneza ni shida ,Bila shaka kuna Vijana wengine hapa wana Magari Mazuri lakini wanayaengesha nyumba ya ng’ambo kwa jirani  kisa hapapitiki”Alisema

Hivyo Waziri Jafo amesema katika kuhakikisha mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania unafanyika bila vikwazo vyovyote ameagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kusimamia vyema ili kuleta ufanisi Mzuri katika utekelezaji wake.

Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema  moja ya hatua ambayo Wizara imefanya ni pamoja na kupitia Sera ya Makazi  ya Taifa ya mwaka 2000 na kupanga  sera Mpya ya Nyumba lengo likiwa ni kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi pamoja na Kuboresha huduma za kijamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi [ESRF]Dkt.Tausi Kida amesema Mnamo Agosti ,2017 Serikali ya Tanzania iliungana na Taasisi hiyo kuanzisha Maabara ya ukuaji wa Miji Tanzania kwa lengo la kusaidia serikali katika uchambuzi mbalimbali wa ukuaji miji huku Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Adolf Ndunguru akishukuru ushiriki wa Taasisi hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad