Waziri kuwachukulia hatua wanaotoa mimba


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile, amesema  Serikali itahakikisha inakomesha uuzaji holela wa dawa mbalimbali,  hususani zile zinazotengenezwa kwa ajili ya matumizi mazuri na kugeuzwa kuwa ni za kutolea mimba.

Waziri Ndugulile ameyabainisha hayo leo Agosti 29,  baada ya Kamati ya Bajeti ya Bunge la Baraza la wawakilishi Zanzibar,  kutembelea Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini Yaani (TMDA).

"Hizi dawa zinazoitwa Misoprostol ni dawa ambazo zinatumika katika uzazi kuongeza uchungu na kupunguza uvujaji wa damu,  lakini dawa hizi hizi katika matumizi yake mabaya zinaonekana zinaweza kusaidia kutoa ujauzito na hilo sasa hivi limeonekana kuwa ndiyo tumizi kuu kuliko lile tumizi la kwanza, lengo na kusudio la dawa lilikuwa ni zuri lakini sasa ni tofauti kwahiyo wajibu wetu kama Serikali ni kusimamia vizuri ". Amesema Dkt Ndugulile.

Aidha Serikali imesema itawachukulia hatua kali zaidi,  wauzaji wote  wanaouza dawa bila kutumia cheti cha daktari na kwamba serikali itaanzisha msako mkali.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad