Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi Wiki ya Uwekezaji

Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi Wiki ya Uwekezaji
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua kongamano la Wiki ya Uwekezaji Kagera leo pamoja na kitabu za mwongozo wa uwekezaji mkoani humo, ambapo jumla ya wadau wa biashara na uwekezaji 300 watashiriki.

Kati ya washiriki hao magavana wa majimbo ya nchi zilizo mpakani mwaka mkoa wa Kagera kutoka Burundi, Rwanda na Uganda pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.

Pamoja na hayo, Mkoa wa Kagera umepanga kuanzia mwezi Novemba kuanza kufanya ziara katika nchi za jirani zinazopakana na mkoa huo, Burundi, Uganda, Rwanda, Kenya na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), kwa ajili ya kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji katika nchi hizo.

Hayo yalielezwa mjini Bukoba jana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akizungumzia kuanza kwa maonesho hayo juzi na maandalizi ya uzinduzi wa wiki hiyo unaofanyika leo mjini hapa.

"Maonesho yanaendelea na yameanza jana (juzi), leo (jana) tunatarajia kupokea wageni kutoka nchi zinazotuzunguka kutoka DRC, magavana kutoka Burundi, Rwanda na Uganda na wafanyabiashara kutoka Rwanda na DRC,"alisisitiza.

Mkuu huyo wa mkoa alisema jambo kubwa ni kwamba leo kutakuwa na ugeni maalumu wa Waziri Mkuu Majaliwa ambaye pamoja na kuzindua rasmi wiki hiyo ya uwekezaji Kagera pia atazindua kitabu maalumu cha mwongozo wa uwekezaji Kagera.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad