Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte kujiuzulu leo
0
August 21, 2019
Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema atajiuzulu baadaye leo kufuatia uamuzi wa chama tawala cha Ligi (League party ) kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani katika muungano huo unaounda serikali.
Italian Deputy Prime Minister and leader of the League party Matteo Salvini gestures while speaking at the upper house in Rome's Palazzo Madama on August 13.
Akilihutubia bunge kuhusiana na mzozo huo wa kisiasa uliozushwa na chama cha Ligi, Conte amesema atakabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella, ambae ataamua iwapo anataka kuitisha uchaguzi wa mapema ama kujaribu kuunda muungano mpya wa serikali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Akiwa mkuu wa nchi Matarrella anaweza kumuomba Conte kuendelea na wadhifa huo na kujaribu kutafuta mbadala wa wingi katika bunge, ama kukubali kujiuzulu kwake na kuangalia iwapo baadhi ya viongozi wengine wanaweza kuunda muungano mbadala wa uongozi.
Ikishindikana, Mattarella anaweza kulivunja bunge, na kuiweka nchi hiyo katika uchaguzi wa mapema mwezi Oktoba.
Tags