Waziri Mwakyembe awataka wasio na kazi mjini warudi makwao


Na. John Walter-Dar es Salaam

Baada ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya kusini Mwa Afrika,Rais wa Awamu ya Tano John Magufuli naye anasubiri kukabidhiwa kijiti hicho.

Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika SADC unaotazamiwa kufanyika  Agosti mwaka huu ambapo Tanzania atakuwa Mwenyeji baada ya takribani miaka 16.

Mkutano Kama huu ulifanyika Tanzania Mara ya Mwisho mwaka 2003/2004 ambapo rais wakati huo Benjamin Mkapa Alichaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa jumuiya Hiyo.

Kufanyika kwa mkutano huo kunatoa fursa mbalimbali kwa wajasiriamali,wafanyabiashara na taasisi za kifedha kutangaza,kuuza na kutoa huduma kwa wageni zaidi ya 800 wanaotarajiwa kuhudhuria.

Waziri anaeshugulikia masuala ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na michezo Dr.Harrison Mwakyembe kuelekea mkutano huo amewataka  watu ambao wapo katika jiji la Dar es Salaam na  hawana  kazi za kufanya warejee makwao kuondoa kero kwa wageni.

“Watu waishi kwa nidhamu ya hali ya juu,wale waliozoea kuingia kwenye mifuko ya watu kuiba iba, hiki sio kipindi chake, waende nyumbani kupumzika, kwa kweli Jeshi la Polisi lisitumie kabisa huruma katika suala hili kwa sababu tunajenga taswira ya nchi, tunataka wageni wakitoka wajue kweli walikuwa kwenye nchi ya amani yenye usalama wa hali ya juu watembee usiku na mchana,”alisema Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe amesema kwa sasa nchi ya Tanzania  inakwenda mbali kwa maendeleo na kasi ni kubwa hivyo ni muda wa kuitambulisha duniani kupitia mkutano huo mkubwa.

Kumbuka kuwa nchi hizi 16 zinazoshiriki katika mkutano huo ambaye mwenyekiti wake kwa sasa ni Rais wa Namibia Hage Geingob,zilikombolewa  kwa mapambano ya silaha nambapo Tanzania ndio ilikuwa kituo kikuu (makao makuu ya OAU liberation Commitee (kamati ya ukombozi)  ya umoja wa Afrika historia ambayo haiwezi kusahaulika.

Mnamo mwaka 2011 African Union iliamua kwamba lazima ijengwe  kumbukumbu kwa ajili ya nchi zote zilizopigania uhuru ambayo itakuwepo nchini Tanzania katika mkoa wa  Dar es Salaam kwa heshima ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Zoezi la ujenzi wa kituo hicho utasimamiwa na wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ambapo wameshaanza taratibu za kutafuta eneo lenye jumla ya hekari 20 ambapo tayari zimeshapatikana hekari 50 katika eneo la Mwage Pande.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe jengo hilo litakuwa na Maktaba,kituo cha habari,kituo cha Tehama,Makumbusho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad