Waziri Ummy, Balozi Misri Wakubaliana Uwekezaji wa Viwanda vya Dawa Nchini

Waziri Ummy, Balozi Misri wakubaliana uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mohamed Gaber Abulwafa na kujadiliana kuhusu kushirikiana katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika mazungumzo hayo pande mbili zimependekeza kushirikiana pamoja katika uwekezaji wa viwanda vya dawa na chanjo, kubadilishana wataalam wa afya ili kuwajengea uzoefu wataalam wetu katika nyanja mbalimbali za sekta nchini.

Pia, Waziri Ummy Mwalimu kwa pamoja wamekubaliana kwa pamoja kuendeleza mapambano ya Homa ya Ini aina C (Hepatitis C) ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora na kwa wakati kuhusu homa ya Ini aina C.

Baada ya majadiliano hayo Waziri Ummy Mwalimu aliagiza kuandaliwa kwa hati ya ushirikiano (MOU) kwa ajili ya kuratibu na kutekeleza maeneo mbalimbali ya kipaumbele katika sekyta ya afya nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad