Yaelezwa mfungwa mmoja ajifungua gerezani bila usaidizi, amshitaki mkuu wa kituo
0
August 30, 2019
Mwanamke mmoja huko Denver, Colorado amemshitaki mkuu wa polisi wa mji huo baada ya kujifungua mwenyewe gerezani bila msaada wa wahudumu wa afya. Diana Sanchez anadai kuwa alilazimishwa kujifungua mtoto wake mwaka jana katika benchi lililokuwa na ubaridi ambalo lilikuwa karibu na choo ndani ya jela. Mwanamke huyo alidai kuwa wahudumu wa gereza hilo walijua kuwa alikuwa anakaribia kujifungua lakini hawakumtilia maanani.
Mkuu wa idara ya polisi ya Denver aliiambia BBC kuwa inafanya uchunguzi ili kubaini wafanyakazi waliokuepo zamu siku hiyo na sababu ya kushindwa kutimiza wajibu wao. Bi Sanchez mwenye umri wa miaka 26 alihukumiwa kwa kosa la wizi wa kitambulisho. Mwanamke huyo alikuwa ameandikiwa siku ya kurudi kujifungua kuwa tarehe 4 Julai 2018 .Na muda ulipowadia , Sanchez alitoa taarifa kwa mtu wa afya kuhusu miadi yake ya hospitali wakati huo alikuwa na mimba ya zaidi ya miezi nane.
Mlalamikaji huyo alisema kwamba tarehe 31 Julai, aliripoti kueleza tena juu ya hali yake na muda wa kujifungua . Alidai kuzungumza na nesi pamoja na mlinzi wa zamu, zaidi ya mara nane majira ya asubuhi, “nilienda kutoa taarifa kuwa uchungu umeanza na hakuna aliyejali”. Kesi hiyo inayodai kuwa mfungwa alijifungua mwenyewe katika gereza kwa saa 5 bila msaada wowote .
‘Kiwewe cha mimba‘
Baadae nesi alikuja kumpima baada ya chupa kupasuka na kumpatia pedi tu, hakufanya jambo lolote lingine na hata kuita gari dharura . “Siku hii ya kujifungua ilipaswa kuwa siku yake yenye furaha zaidi lakini ilibakia kuwa siku yenye hofu, maumivu na udhalilishaji uliopelekea kupata kiwewe cha mimba”.
Kwa mujibu wa BBC. Msemaji wa kituo hicho cha polisi kuwa gereza lao lina lina huduma zote za afya na wanafanya kazi kitaaluma , kuna vifaa vyote vya huduma ya afya katika jela hiyo. “Huwa tunaelewa hali wanayopitia wajawazito wote walioko jela pamoja na Sanchez mwenyewe, ndio maana tuna kitengo maalum cha afya ambacho kinafanya kazi kwa weredi. Lakini kuhakikisha kuwa tukio kama hilo halijirudii, mkuu wa kitengo amebadilisha utaratibu kuwa mtu yeyote mwenye ujauzito gerezani akifikia muda wa kujifungua, atapelekwa hospitali badala ya kuhudumiwa hapo”.Madai hayo yamepelekea maafisa wa liopelekea uzembe huo kutokea kuwajibishwa.
By Ally Juma.
Tags