Yanga SC Kula Bata Mwanza

YANGA itafanya ziara yake jijini hapa kuanzia Jumatano ijayo na itacheza michezo miwili ya kirafi ki ikiwa ni pamoja na kushiriki shughuli za usafi jijini hapa. Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga Mkoa wa Mwanza, Mhando Madega alisema;

“Timu yetu ikiwa hapa tutakuwa tukifanya shughuli za usafi lakini pia timu itapata muda wa kucheza michezo miwili ya kirafi ki ambayo itakuwa na lengo la kuichangia timu hiyo fedha ili iendelee kuimarisha mfuko wake kwa kuwa tunakabiliwa na mashindano ya kimataifa.”

Madega ameongeza kwamba Yanga itacheza mchezo wa kirafi ki dhidi ya timu moja kutoka Kenya ambayo bado wanafanya nayo mazungumzo. Madega amewaomba wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad