Yesu feki Aliyedaiwa Kufa Bado Yupo Hai Nchini Kenya

Mhubiri wa Marekani na muigizaji, Michael Job, ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Kenya na kuitwa 'Yesu bandia' hajafariki kama ilivyotangazwa hapo jana na vyombo vya habari na mitandao.

Kulingana na uchunguzi wa BBC Swahili Mhubiri huyo yupo hai na mzima wa afya, pia yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa awali.

Taarifa za vyombo vya habari zilianza kuenezwa kuwa Yesu huyo bandia alifariki siku chache tu baada ya kuhudhuria ibada ya kidini. Inadaiwa kwamba alifariki siku chache tu baada ya kutembelea taifa hilo la Afrika mashariki baada ya kuuguwa ugonjwa wa mapafu.

Hata hivyo mhubiri huyo ameendelea kuchapisha picha na video za shughuli zake siku baada ya siku. Katika chapisho hilo na kanda za video alizoweka katika akaunti yake ya facebook Bwana Job anaonekana katika gari moja akihubiri Kiingereza huku akisaidiwa na mkalimani huku watu wakifuatilia mahubiri yake.

Hii sio ziara yake ya kwanza barani Afrika, mapema mwaka huu alikuwa nchini Togo, licha ya kwamba picha alizoweka kutoka huko hakuonekana akiwa amevaa mavazi ya kuiga, bali alikuwa amevaa suti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad