Yoweri Museveni na Paul Kagame wasaini makubaliano kumaliza mgogoro baina ya Uganda na Rwanda


Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.

Walifikia makubaliano hayo katika mkutano wa pili huko Luanda mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo , Angola na rais wa Congo Brazaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Joto la kisiasa limekuwepo kwa takriban miaka mitatu sasa na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.


Maafisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

"Tutashughulikia matatizo haya yote". rais Kagame amewaambia wandishi habari baada ya kusaini makubaliano hayo.

Ruka ujumbe wa Twitter wa @NewTimesRwanda

The New Times (Rwanda)

@NewTimesRwanda
 President #Kagame and President Museveni today signed a MoU in an effort  to resolve the ongoing standoff between #Rwanda and #Uganda.

Details of the MoU👇🏿

View image on TwitterView image on Twitter
158
4:23 PM - Aug 21, 2019
Twitter Ads info and privacy
73 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @NewTimesRwanda
Makubaliano ya leo yamefikiwa baada ya "jitihada zilizoidhinishwa na Angola kwa usaidizi wa DR Congo" kwa mujibu wa ikulu ya Angola.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kutilia mkazo kutatua mzozo wowote baina ya mataifa yao kwa njia amani shirika la habari nchini Angola, Angop linaripoti.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alhmd Lillah.
    kwisha kwake ndiyo udumishaji wa Ujiraani mwema na Udugu.
    Afrika na watu wake ni wamoja.

    Heshima / Amani na Udugu ndiyo ngao zetu na Msimamo wetu.

    Mungu Ibariki Africa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad