Zahera Ajitete Baada ya ‘Kupigwa’ na Polisi


Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga, Mwinyi Zahera wakati akielezea baadhi ya sababu zilizopelekea timu yake kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania kwa kufungwa magoli 2-0 jana kwenye uwanja wa Ushirika-Moshi, amesema.

“Tatizo la kwanza lilikuwa ni uwanja, wachezaji wengi tuliowatumia kwenye mchezo dhidi ya Polisi  Tanzania wanachezea sana mpira lakini kutokana na hali ya uwanja ilikuwa ni ngumu kuona pasi tatu…mpira unapigwa tu mbele hilo lilikuwa tatizo kwetu.”

“Kikosi ambacho kitacheza mchezo dhidi ya Township ni tofauti na ambacho kimecheza na Polisi Tanzania. Tunapowapa nafasi wachezaji kwenye mechi kama hizi wanatakiwa kuonesha uwezo lakini kuna baadhi ya wachezaji itakuwa ngumu kucheza kikosi cha kwanza cha Yanga msimu huu.”

“Jambo hili wachezaji wanapaswa kulijua, hii imekuwa mara ya pili mara ya kwanza tulikuwa Zanzibar tukachezesha vikosi viwili. Kikosi cha kwanza kilicheza kipindi cha kwanza kikafunga magoli matatu. Kipindi cha pili tukabadili timu nzima.”

“Mechi ya pili Zanzibar wakacheza dakika 90 wale waliocheza kipindi cha pili mechi ya kwanza wakatoka sare ya kufungana 1-1, dhidi ya Polisi Tanzania wamecheza tena lakini wengine wanaoekana itakuwa ngumu kupata nafasi kwenye mchezo wa marudiano na Township Rollers.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad