Zahera akomaa na washambuliaji Yanga



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametumia zaidi ya dakika 50 kuipa timu yake mazoezi tofauti ya mbinu za kufunga.
Katika mazoezi yaliyofanyika leo Jumamosi asubuhi Uwanja wa Chuo cha Polisi, Zahera alianza na ratiba ya mazoezi ya pumzi kwa wachezaji kukimbia mbio kali wachezaji wakigawanywa katika makundi mawili tofauti.
Baada ya mazoezi hayo ya pumzi Zahera alibadilisha zoezi akihamia mazoezi ya kutengeneza nafasi ya kufunga.
Mazoezi hayo yalikuwa yanaanzia katika nafasi ya kiungo ambapo viungo hao wakiongozwa na Papy Tshishimbi, Feisal Salum, Mapinduzi Balama wakipewa mbinu za kuanzisha mashambulizi kwa viungo wa pembeni

Viungo wa pembeni Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana na Issa Bigirimana nao walitakiwa kuwa kukimbia na pasi hizo kutoka kiungo cha kati na kupiga krosi au kufunga.
Kazi ya kufunga ilikuwa chini ya Juma Balinya, Sadney Urikhob na David Molinga.
Hata hivyo mwanzo wa mazoezi hayo washambuliaji hao walionyesha uwezo duni wakishindwa kumalizia vyema kwa mashuti yao kupanguliwa na makipa Farouk Shikhalo na Ramadhan Kabwili.
Hali hiyo ilamlazimu Zahera na msaidizi wake Noel Mwandila kukatisha zoezi hilo mara kadhaa na kuwapa maelekezo zaidi ambapo baadaye hali ilibadilika na kuanza kufungwa kwa mabao.
Washambuliaji na viungo ambao wakionekana kufanya vizuri ni Molinga, Balinya, Deus Kaseke, Mrisho Ngassa na hata Bigirimana ambao wakifunga mara tano kila mmoja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad