Zahera amtolea uvivu Lwandamina kisa kaifundisha Yanga


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema haofii chochote kuelekea kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza wa  klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Zesco United kutoka Zambia.

Zahera ameyasema hayo kupitia kipindi cha Yanga Tv kilichorushwa na Azam Tv hapo jana saa 1 : 00 usiku na kuongeza kitendo cha Georg Lwandamina kuwahi kuifundisha Yanga SC hakimnyimi usingizi kuelekea mechi hiyo.

Zahera amtolea uvivu Lwandamina kisa kasikia kafundisha Yanga, aitaja Simba ”Ya leo sio ya kesho na ya kesho sio ya leo, Ailete tu Zesco

”Kocha yule kuwa amepita Yanga SC, ile ilikuwa yazamani hata wachezaji wengi aliyowahacha hawapo tena. Mpira una mambo mengi ya leo sio ya kesho na ya kesho sio ya leo.

”Alipita Yanga, alishapita hapa sasa ni Zesco dhidi ya Yanga ndiyo watacheza, sisi tunamipango yetu na wao wanampango yao.

Zambia nchi ambayo inatoka klabu ya Zesco United inashika nafas ya 81 katika ubora wa viwango vya soka duniani wakati Tanzania inapotokea Yanga SC ipo kwenye nafasi ya 137.

Katika hilo Zahera amesema haitoshi kuwa sababu ya timu yake kuihofia Zesco ”Mpira wa Congo, Misri na Algeria ni mkubwa kushinda wa Tanzania ?, Simba aliwapiga hapa wa Misri, alimpiga Vita Club na aliipiga timu ya Algeria hapa na mpira wao mkubwa kuliko wa Tanzania, sasa sijajua namna gani Yanga asimpige Zesco.”

”Hatakama Zambia ina ligi bora sisi hatuwezi kuogopa timu kama Zesco, hatuwezi tunacheza mpira tukiwa na lengo moja na inawezekana.”

Yanga inaweka kambi jijini Mwanza ambapo itacheza mechi mbili za kirafiki ambazo ni  Mbao FC na Pamba Sports Club ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na mkondo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United kutoka Zambia itakayochezwa siku ya Jumamosi tarehe 14 ya mwezi ujao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad