Zimbabwe Yapinga Tamko la Nchi za Ulaya....Yasema Kamwe haitaruhusu tishio la mapinduzi linalotolewa na upinzani


Serikali ya Zimbabwe imesema, haitaruhusu tishio lolote linalotolewa na upande wa upinzani la kupindua serikali, huku ikisisitiza kwamba raia wana haki ya kikatiba lakini hawapaswi kukiuka haki za wengine.


Tamko hilo la serikali limekuja baada ya Umoja wa Ulaya na nchi nyingine za magharibi zikiwemo Uingereza na Marekani kutoa taarifa ya pamoja hapo jana, ikiilaumu serikali ya Zimbabwe kwa madai ya kukiuka haki za binadamu wakati wa maandamano yaliyoongozwa na kundi la upinzani huko Harare tarehe 16 mwezi huu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad