Afisa wa polisi ametimuliwa kazi baada ya kuwakamata watoto wawili wa miaka sita, fahamu zaidi

Afisa wa polisi nchin Marekani ametimuliwa kazi baada ya kuwakamata watoto wawili wa miaka sita. Watato hao walikamatwa shuleni katika mji wa Orlando, jimboni Florida.



Mmoja wa watoto hao alifungwa pingu baada ya kufanya fujo na kumpiga mateke mwalimu wake, bibi wa mtoto huyo ameviambia vyombo vya habari.

Afisa Dennis Turner, amefutwa kazi baada ya viongozi wake kudai hakupata ruhusa stahiki kabla ya kuwakamata watoto hao.

Waendesha mashtaka wamesema wataifuta rekodi hiyo ya kumatwa kwa watoto hao.

Watototo wote wawili walikamatwa kwa mashtaka ya shambulio.

“Watoto hawa hawatashtakiwa, na pia naangalia juu ya namna ya kufta rekodi hii kabisa ili isiharibu mustakabali wao wa maisha,” mwanasheria wa serikali Aramis Ayala amewaeleza wanahabari.

Mkuu wa polisi wa Orlando Rolón amesema: “Nikiwa kama babu wa wajukuu watatu walio chini ya miaka 11, tukio hili linanigusa sana. Kikosi chetu kinajitahidi kuwa na weledi na kuihudumia jamii katika njia bora.”

“Tulipokwenda kumtoa polisi, walituambia tusubiri kidogo sababu walikuwa wakichukuliwa alama zao za vidole, na niliposikia hivyo, ilikuwa kama nimedondoshewa tani ya matofali,” ameelezea bibi wa mtoto mmoja.

“Mtoto wa miaka sita hatakiwi kusema kuwa alifungwa pingu, na kupakiwa nyuma ya gari la polisi, na kupelekwa mahabusu ya watoto ili kuchukuliwa alama za vidole na kupigwa picha.”

Kwa mujibu wa polisi, afisa Turner alikuwa ameondolewa kwenye kikosi cha polisi na alikuwa akifanya kazi ya ulinzi shuleni kama askari wa akiba.

Shule nyingi nchini Marekani zimekuwa zikiajiri askari wa akiba kama walinzi baada ya kukithiri kwa mashambulio ya risasi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AFP asilimia 46 ya shule zote marekani zinalindwa na afisa walau mmoja kwa kila siku.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad