Manusura wa ajali ya lori la mafuta mjini Morogoro waliokuwa wamelazwa Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi Mganga mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Kusirye Ukio manusura wanane kati ya kumi na wanane waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo wameruhusiwa kutoka wodini baada ya hali yao kuimarika.
Mwanafunzi atua ndege baada ya mwalimu kuzirai
DK. Ukio amesema wagonjwa hao walianza kuruhusiwa kwenda nyumbani wiki iliopita na kwamba ku10 waliosalia wanaendelea kupewa matibabu chini ya uangalizi wa wauguzi na madaktari.
Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo ya Agosti 10,2019 mjini Morogoro imefikia watu 104.
Kiwango hicho cha vifo kilitokana na majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuendelea kuaga dunia.
Watu 62 walithibitishwa kufariki siku ya mkasa na zaidi ya 70 kujeruhiwa, na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu mpaka leo hii Septemba 1, 2019.
Mapema wiki iliyopita BBC iliripoti juu ya majeruhi 13 wa ajali hiyo waliosalia hospitali ya taifa hilo Muhimbili, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbo na viungo vyao.
Daktari Bingwa wa Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Edwin Mrema alieleza kuwa upasuaji unaweza kufanyika ndani ya wiki mbili au tatu ikitegemea na ukubwa wa mtu alivyoumia.
"Ile ngozi imekufa hivyo lazima itoke kwa dawa na kila siku tunasafisha kwa usafi kabisa.
Wiki mbili mpaka tatu , inategemea ule unene wa kuungua au athari ya moto imeenda chini kiasi gani?"
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema kuwa kati ya majeruhi 13 sasa wamebaki 11 baada mmoja kufariki tarehe 31 Agosti na mwingine tarehe 28.
Ajali ya Morogoro: Manusura waruhusiwa kutoka hospitali
0
September 02, 2019
Tags