Msanii wa Bongo Fleva, AliKiba amewashauri wanafunzi wa kidato ch Nne katika Shule ya Secondari ya Dunga kujikita zaidi katika masomo na kuacha kufanya mambo yasiyofaa.
Alikiba aliwaambia wanafunzi hao ili kufikia mafanikio katika maisha yao wanatakiwa kuongeza bidii katika masomo yao na kufanya vizuri katika mitihani yao.
Hayo aliyaeleza leo huko wilaya ya Kati Unguja wakati alipokwenda kuwatembelea wanafunzi wa kidato cha Nne shule ya Sekondari ya Dunga ambao wanaotarajia kufanya mitihani ya taifa mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema kuwa mafanikio katika maisha yanapatikana endapo wanafunzi watazingatia masomo nakuacha mambo ambayo hayana umuhimu yakiwemo mapenzi.
“Ndugu zangu wanafunzi leo nipo hapa na nyinyi kuwashauri kuwa muongeze bidii katika masomo yenu, najua kuwa hapa kuna Marais wa baadae, wabunge na hata wawakilishi kama Mhe, Simai lakini humu ndani naona Sura za wasanii wengi hivyo someni sana taifa linawategemea” alisema AliKiba.
Kwa upande wake Naibu wa Wiziri wa Elimu Zanzibar Simai Muhamed Said aliwaahidi wanafunzi hao kuwa kwa atakayefaulu wa daraja la kwanza atampatia Tsh. Milion 1 na ufaulu wa daraja la Pili atapata 500,000.