Baada ya Kuagwa Mwili wa Mugabe Kuzikwa Baada ya Mwezi

Mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe umehifadhiwa katika eneo alilozaliwa mara baada ya watu kumuaga katika mji mkuu wa Harare.

Viongozi wa Afrika wamemsifu aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama mpiganiaji wa Uhuru katika mazishi yake katika uwanja wa kitaifa mjini Harare.

Rais wa sasa Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia'.

Hatahivyo uwanja ulio na uwezo wa kubeba watu 60,000 ulikuwa na idadi ndogo ya watu.


Raia walikuwa upande mmoja wa uwanje huo
Uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.

Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira ni baadhi ya masuala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe.

''Tunafurahia kwamba amefariki, kwa nini nihudhurie mazishi yake? sina mafuta'', alisema mkazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP.

''hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. yeye ndio sababu ya matatizo yetu''.


Mazishi hayo yanafuatia mgogoro kati ya familia ya Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa.

Sasa imekubalika kwamba atazikwa katika makaburi ya mashujaa mjini Harare, familia yake imesema.

Msemaji wa familia na mpwa wake leo Mugabe anasema kwamba hiyo itafanyika baada ya kipindi cha mwezi mmoja wakati ambapo kaburi hilo litajengwa katika makaburi hayo ya mashujaa .

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad