Baada ya Msamaha wa Rais, Ngeleja Aongea


Mbunge wa Sengerema William Ngeleja amesema kuwa, amefurahishwa na hatua za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kumsamehe yeye pamoja na wabunge wengine.


Ngeleja amesema kupitia msamaha huo, amepata faraja kwa kuamini kuwa msamaha huleta faraja kwa maisha ya mwanadamu.

Ngeleja ameyabainisha hayo leo Septemba 12 katika kikao cha Bunge mjini Dodoma, ambapo amepata fursa ya kumshukuru  Rais Magufuli kwa hatua hiyo aliyoifanya dhidi yao, hii ni baada ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, kuwapongeza kwa hatua ya kumuomba radhi Rais Magufuli.

''Mimi natumia nafasi hii na kwa niaba ya wapiga kura wa Jimbo la Sengerema kuelezea faraja niliyonayo ya kupata msamaha, na naamini kuwa Mwenyezi Mungu atazidi kumjalia Mh Rais'' amesema Ngeleja.

Hatua hii imekuja ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais Magufuli, alipoamua kuwasamehe wabunge hao, akiwemo January Makamba na Nape Nnauye, mara baada ya kuvuja kwa sauti zao na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zilizosikika zikitoa maneno yasiyofaa dhidi ya Rais Magufuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad