Bahamas yapigwa na kimbunga kibaya zaidi


Kimbunga chenye nguvu zaidi kimepiga visiwa vya Bahama nchini Marekani na kuvunja rekodi za vimbunga vyote vilivyowahi kupiga na kusababisha maafa makubwa .

Hii ni dhoruba ya pili katika rekodi ya bahari ya atlantiki ambayo imeweza kustahimili mawimbi mpaka kufikia 175mph (285kilometa kwa saa).

Kimbunga hicho kinaendelea kusonga taratibu magharibu na kinaweza kufika mashariki ya bahari ya Marekani, majimbo ya Marekani ya Florida, Georgia na South Carolina yote .

Dhoruba hii inavuma vya kasi ndogo ambayo inasafiri toka magharibi ambayo ni kilometa 9 kwa saa ambayo ni sawa na mph 6.

Mwanafunzi atua ndege baada ya mwalimu kuzirai
‘Lango la jehanamu’ lafungwa baada ya watalii kufariki
Haki miliki ya pichaAFP
Lipi jipya kutoka Bahamas?
Kituo maalum cha janga la kimbunga kimesema kuwa kimbunga hicho kilipiga majira ya saa kumi, dhoruba hiyo ilitokea pembezoni mwa mashariki mwa Bahama, na kutua katika kisiwa cha Abaco.

Grand Bahama ina jumla ya idadi ya watu ambayo ni takribani 50,000, wanaoishi umbali wa kilometa 100 mashariki magharibi mwa pwani ya Palm huko Florida.

'Ni dhoruba yakutishia maisha' ambayo ipo katika futi 23 ambayo ni sawa na mita 7 kama inavyokadiriwa katika baadhi ya maeneo.

Mpaka sasa hakuna kauli rasmi kutoka kwa maafisa wa visiwa vya Bahamas juu ya majanga hayo.

Ingawa kuna ripoti ambayo imetolewa kuwa maeneo yaliyoathirika Bahamas yanakumbwa na changamoto ya umeme na shida ya mtandao.

Hata hivyo, video na picha zilizotumwa katika mtandao wa Twitter na Bw. Latrae Rahming ambaye ni msaidizi wa waziri mkuu mstaafu Perry Christie, zinaonesha maafa makubwa katika visiwa vya Abaco, ambayo ni makazi ya takribani watu 17,000.

Magari yamejaa maji, paa zimeharibiwa na maji ya pwani ambayo yamefikia ukingo wa paa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad