Barca Yamkazia Messi, Kumpa Mkataba Mpya

Barca yamkazia Messi, kumpa mkataba mpya
Klabu ya Barcelona ya Uhispania, inatarajia kumtia kitanzi kingine mshambuliaji wao hatari kwa kutupia Lionel Messi mwenye umri wa miaka 32.

Mabosi wa klabu hiyo wanataka kumuongezea mkataba ambao utambakiza Messi ndani ya Neo Camp kwa miaka iliyosalia ya soka lake.

Rais wa Barcelona Jose Maria Bartomeu amesema kuwa, Messi anatarajia kumaliza mkataba wake na utamruhusu yeye kuondoka Barcelona bure.

Barcelona wanaamini kuwa watambakiza nyota huyo hadi 2022 na baada ya hapo sasa ataruhusiwa kuondoka Neo Camp. Inadhaniwa kuwa huenda nyota huyo atarudi kucheza nchini kwao Argentina kunako klabu yake ya zamani ya utotoni Newll's Old Boys kabla ya kustaafu kandanda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad