BREAKING: Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Tundu Lissu Kupinga Kuvuliwa Ubunge

 

Mahakama Kuu Kanda ya Dar, imetupilia mbali maombi ya Tundu Lissu kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge kwa maelezo kuwa alipaswa kuweka pingamizi dhidi ya uchaguzi na si kuomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Spika.


Imedaiwa maombi hayo yangesikilizwa hadi mwisho na Lissu kushinda, Jimbo la Singida Mashariki lingekuwa na wabunge wawili ambapo ni kinyume cha Katiba. Pia maombi hayo yemechelewa kuletwa mahakamani.


Akitoa uamuzi huo Jaji Sirilius Matupa leo Jumatatu Septemba 9, amesema maombi ya Lissu hayatekelezeki kwa sababu mleta maombi alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi mahakamani badala yake wameleta maombi ya kutaka kupinga uamuzi wa spika.


“Mahakama imepata wakati mgumu sana katika kupitia maombi haya kwa sababu kilichotakiwa ni kupinga uchaguzi na lakini hakuna mahali walikofungua kesi mahakamani.


“Tungeruhusu maombi haya hadi mwisho, maana yake Singida Mashariki ingekuwa na wabunge wawili kitu ambacho ni kinyume na Katiba,” amesema Jaji Matupa.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bombaaa!!
    Lissu, mwanasheria, hata hilo la kupinga uchaguzi mahakamani hukulijua?!!
    HONGERENI SINGIDA MASHARIKI kuondokana na magumashi.
    UsirudieKosaKupigiaKuraUpinzaniOvyo!

    ReplyDelete
  2. Alifikiri kodi zetu atazila Dezo..!!!
    Uwakilishi Magumashi haupo tena.

    Hivyo alivyokkuwa mwakilishi enzi zile Mshahara sikaribia laki 2..!!! kwa mwezi na Hazina Makato TRA.

    Mjasili amali analipa kitambuli elfy 20. huyualikuwa analipa napi? Au shambala bibi...!!! ?

    ReplyDelete
  3. Alifikiri kodi zetu atazila Dezo..!!!
    Uwakilishi Magumashi haupo tena.

    Hivyo alivyo kuwa mwakilishi enzi zile Mshahara si karibia laki 2..!!! kwa mwezi na Hazina Makato TRA.

    Mjasili amali analipa kitambulisho elfu 20. huyu alikuwa analipa ngapi? Au ilikuwa shamba la bibi...!!! ?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad