BREAKING: Kampuni ya Mawasiliano MTN Ya Afrika Kusini Yafunga Maduka yake Nigeria

KAMPUNI la mawasiliano la Afrika Kusini la MTN, limetangaza kufunga maduka yake yote nchini Nigeria kutokana na baadhi ya raia wa Nigeria kulipiza kisasi cha mashambulizi ya kibaguzi yanayofanywa dhidi ya raia wa Nigeria walio nchini Afrika Kusini.
Mashambulizi hayo yamemfanya Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria,  Geoffrey Onyeama, kusema kwamba serikali ya Afrika Kusini haijachukua hatua za kutosha kumaliza tatizo hilo.

Mashambulizi hayo yamewafanya baadhi ya raia wa Nigeria kuchoma moto baadhi ya makampuni ya Afrika Kusini yakiwemo ya  MTN, Dstv, na Shoprite.

Kampuni la MTN leo (Jumatano) llimeandika ujumbe kwa wateja wake mtandaoni kuwajulisha kufungwa kwa kwa maduka yake.

Ujumbe huo uliandikwa:
”Yello! Our shops are unavailable today. You can reach us on Twitter- @MTN180, MTNonline.com/Livechat, chat on MyMTN App. For Call Center dial 180.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad