BRELA watoa mafunzo kuhusu utoaji wa Leseni za Biashara

Kufuatia kauli mbiu ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli inayosema Tanzania ya uchumi wa viwanda wakala wa usajili wa leseni za biashara na makampuni  “BRELA”  wametoa mafunzo kuhusu utoaji wa leseni za biashara kwa mfumo wa kielektroniki “NATIONAL BUSINESS PORTAL” katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba  Mkoani Kagera.

Nae Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Denis Mzamiru amefafanua kuhusu mfumo huo kuwa ni moja ya jitihada za awamu ya tano ili kuwawekea urahisi wa mazingira ya biashara kwa wafanya biashara ya ndani na nje.

“Kama mnavyojua Tanzania ni nchi ya kibiashara pia hata sisi tumeona mfumo huu utarahisisha taaraifa za mfanyabiashara hata hivyo tunalazimika kuweka taarifa za biashara katika mtandao vilevile tumepunguza changamoto kwa wafanya biashara kuacha kwenda umbali mrefu hili kupata lesseni pia itapunguza mianya yaa rushwa kupitia mifumo hii pamoja na kupanua wigo wa serikali katika kupata mapato zaidi”

Hata hivyo,  Ndg. Merkisedek Kalinga kwa niaba ya Afisa biashara wa mkoa ambae pia ni mchumi amewasisitiza wafanya biashara walioudhuria mafunzo hayo kuwa mfumo huu utawasaidi zaidi hata katika upatikanaji wa taarifa zao katika kupitia mfumo huo mda wowote na pia itakuwa rahisi kupata leseni kwa haraka kuliko kukaa kusubili leseni wakati huo biashara ya mfanyabiashara imesimama.

Vilevile mafunzo hayo yamewashirikisha wadau mbalimbali wa biashara na makampuni wakiwemo wadau wa Bank ya NMB ambao wao ndio watu ambao leseni za wafanya biashara zinapita mikono yao wakati wakiwa wanalipia biashara zao.

Aidha nae mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba yalipo fanyika mafunzo hayo Mh. Limbe Molis ametoa wito kwa wafanya biashara kuchangamkia fursa hiyo kwa kusajili biashara zao na kukata leseni kwa mfumo wa kielektroniki “NATIONAL BUSINESS PORTAL”huku akiwashukuru wakala wa  leseni BRELA kwa kutoa mafunzo ambapo itachangia kukuza pato la mkoa pia.

Sambamba na hayo naobaadhi ya wafanya biashara  mkoani humo wameupokea vizuri mfumo huo huku wakioji na kuwataka wakala wa BRELA kutoa elimu zaidi ili kuwapa uelewa mpana wafanya biashara na wamiliki wa makampuni mbalimbali hili kuongeza pato la taifa ikiwa mafunzo ya mfumo huo yanatolewa katika wilaya sita nchi nzima
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad