Bunge lampongeza Rais Magufuli kuwa kwenye Mwenyekiti wa SADC

Bunge limewasilisha azimio la kumpongeza Rais John Magufuli kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Azimio hilo limewasilishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan (Zungu) ambaye amesema wanafanya hivyo kwa dhati kabisa na kwa umoja.

"Tunampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa kutoa wito kwa nchi wanachama kuimarisha viwanda vyao ili kuweza kuzalisha bidhaa ambazo watashirikiana kununua na kuuza ndani ya nchi za SADC badala ya kuagiza kutoka nje,” amesema Zungu.

Ameendelea kwa kusema, "Kwa kuwa tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, mataifa mengi yamekuwa yakipendezwa na uongozi wake na kutokana na kuaminiwa na viongozi wote wa nchi za SADC waliamua kumpa uenyekiti wa nchi hizo hivyo bunge linaazimia kwa kauli moja kumpongeza,”.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad