DC Aomba Radhi Kumzushia Kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela, amelazimika kuomba radhi kwa umma, baada ya kusambaza taarifa za uongo juu ya kufariki kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim.

Hapo jana usiku Kasesela alichapisha taarifa kwenye mtandao wa Twitter, ukieleza kutokea kwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim zilizodai kuwa mauti hayo yamemfika akiwa nchini Uingereza, ambapo  baadae alizikanusha.

"Kwa dhati naomba nimuombe radhi, Dr. Salim Ahmed Salim na kwa sasa bado yuko na anaendelea na matibabu nchini Uingereza nimeongea na familia, ni bahati mbaya sana chanzo kilichonipa habari hakikuwa sahihi, ninaomba radhi kwa familia na Watanzania kwa ujumla."ameandika Kasesela.

Mapema jana Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping alimtunuku Waziri Mkuu huyo mstaafu  wa Tanzania Dkt Salim, kuwa miongoni mwa watu waliosaidia nchi hiyo kurejeshwa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad