DC Jokate amkabidhi nyumba mwanamke aliyejifungua mapacha katika mazingira magumu


July 12 mwaka jana (2018) Ester Simon mkazi wa kijiji cha Mzenga, wilya ya Kisarawe mkoani Pwani alijifungua watoto wawili mapacha walioungana tumboni. Mama huyo (24) alijifungua kwa masaada wa mkunga wa jadi na baada ya kuona watoto hao wameungana walipelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili. Baada ya uchunguzi ilionekana 'wanashare' baadhi ya viungo vyao vya mwili ikiwemo ini.

Hata hivyo September 22, 2018 walifanikiwa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha kwa gharama ya shilingi milioni 34 ambazo zililipwa na United Bank of Afrika kwa kuwa mama huyo hakuwa na uwezo wa kumudu.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo aliwatembelea watoto hao na kuahidi kuwajengea nyumba bora ya kuishi. Jokate alitafuta wafadhili (Africanreflectionsfoundation) waliomjengea nyumba ya kisasa ya vyumba viwili, veranda, sebule, etc ambayo ameikabidhi leo.

Pia Jokate amefanikiwa kuwatafutia watoto hao wafadhili waliowasaidia bima za afya kwa miaka 10. Amewafungulia pia akauti BOA bank ambapo benki hiyo imewawekea kiasi cha shilingi milioni 2 kama kianzio, na kufungua dirisha kwa wasamaria wema kuendelea kuchangia. Hospitali ya taifa Muhimbili nayo imekubali kuwahudumia bure watoto hao kwa kipindi cha miaka mitano, ikiwa watapata changamoto zozote za kiafya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad